Wednesday , 4th Nov , 2015

Msanii anayewakilisha vyema pande za Mbeya Izzo Bizness amesema hatarajii kuingia kwenye maisha ya ndoa hivi karibuni, ingawa yuko kwenye mahusiano.

Izzo Bizness amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwamba mipango ya ndoa itafanyika muda muafaka utakapofika, lakini kwa sasa hawezi kuingia kwenye ndoa kwa kuwaridhisha watu.

"Umri unaenda lakini ndoa ni mipango, siwezi kuoa kwa kuwaridhisha watu kwa kuwa mimi ni kioo cha jamii, si kitu rahisi kama watu wanavyofikiria ingawa niko kwenye mahusiano", alisema Izzo Bizness.

Izzo Bizness aliendelea kusema kwamba kwa sasa anajali zaidi mazingira ya mtoto wake ili asije akayapitia yale aliyoyapitia yeye, ingawa suala la ndoa ni lazima.

"Nina mtoto mmoja anaitwa Pouline nampenda sana, sihitaji kuja ku-experince vitu ambavyo nime experience akaja kuja kuexperience mtoto wangu, lazima nimtengenezee future, lazima nihakikishe ataenda shule nzuri, elimu bora, na tunafahamu gharama za watoto kuhusu shule, kwa hiyo nina muda mwingi sana wa kukaa na kupanga kwanza maisha ya mtoto ingawa ndoa ni lazima lakini kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia", Alisema Izzo Bizness