Friday , 17th Jul , 2015

Staa wa muziki wa Bongofleva Izzo Bizness ameweka wazi furaha yake ya kushirikiana na staa nyota wa muziki wa nchini Uganda Navio baada ya kufanya naye kolabo ya remix ya wimbo wake 'Walala Hoi '.

Staa wa muziki wa Bongofleva Izzo Bizness

Mbali na hilo Izzo ameongea na eNewz kuwa yupo mbioni kuachia kazi zake mbalimbali na kusema kuwa kazi yake ya Walala Hoi Remix inatarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali akiwa na nyota huyo wa Uganda.