Akizungumza na eNEWZ ya Eatvz, Isha amesema kwamba wasanii wa kitanzania kuvaa mavazi yanayowafanya waonekane utupu kwa madai ya kutafuta soko la kimataifa wanajidanganya kwani kinachoouza siyo video bali ni meseji ya kitu kinachoimbwa.
Isha amedai kwamba video zinasaidia kuwatambulisha wasanii katika jamii ili waweze kufahamiana na mashabiki zao lakini haimaanishi kwamba wavae nguo za uchi katika video zao kwa kuwa hazitoweza kuwasaidia chochote katika maisha yao ya sanaa.
"Tunaiga sana. Hatukatazwi kuiga lakini sisi tumekuwa tukiiga kupitiliaza sana kitu ambacho wakat mwingine kimekuwa kinatia aibu Unaweza ukawa unatazama wimbo na mkwe wako hapo hapo unakuta mtu mavazi alivovaa yanatia aibu . Hapo inabidi ugeuze shingo kati yako au mkwe wako na mkikuta mmeangaliana uso kwa macho ndo haya tena" amesema Bi. Isha.
Hata hivyo Isha amewasifia wanamuziki wa Taarabu kwa kusema mara nyingi wamekuwa wakiva mavazi ya stara tofauti na wasanii wengine wote na kuwashauri wasanii wengine kutoogopa kuvaa kama wao kwa kuhofia mashabiki au video zao kuacha kuchezwa kwenye Televisheni.


