.jpg?itok=-0d9J4wL×tamp=1473258252)
Peter Msechu ameyasema hayo alipokuwa akiutambulisha wimbo huo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa alivyoutuma wimbo huo kwa baadhi ya media zilizopo nchini Nigeria, wengi waliukubali wakidhani umetengenezwa na Producer Shizzy.
“Unajua nilipoutuma kwenye baadhi ya media Nigeria wengi walishtuka, unajua pale nilipomtaja producer Teaz watu wakajua ni Shizzy yule producer wa Davido, kwa hiyo imekuwa nzuri sana naikubali mwenyewe, na imepokelewa poa”, alisema Peter Msechu.
Peter Msechu ameendelea kusema kuwa alikuwa na kazi kubwa sana ya kuhakikisha wimbo atakaoutoa unapita ule wa nyota, na anajiandaa kwenda kufanya video yake wiki ijayo.
“Wiki ijayo nitaenda kufanya video na nimeshailipia kila kitu, nikamwambia producer tusidaiane.. niko vizuri baba watu wasubiri tu”, alisema Peter Msechu.