Thursday , 3rd Apr , 2014

Staa wa muziki wa nchini Nigeria, Ice Prince ameweka wazi kuwa, katika historia ya maisha yake, alikwishawahi kubakwa akiwa na umri wa miaka 13 tu, na mwanamke ambaye alikua anamchukulia kama anti yake, ambaye alikuwa akiishi jirani na familia yao.

Ice Pronce

Ice Prince anasema kuwa, hii ni kumbukumbu mbaya kabisa kwake, na kila anapofikiria anajisikia vibaya, na msanii huyu kwa maoni yake amesema kuwa, mapenzi sio kitu kizuri kama watu wanavyoyachukulia.

Ice Prince kuhusiana na tukio hili amesema kuwa, hakupenda kuliweka wazi kwa mtu yoyote baada ya kumtokea, na tangu wakati huo, hakuwahi kumuona tena mwanamke huyu aliyemfanyia kitendo hiki cha kusikitisha.

Tags: