.jpg?itok=g8JSvHwC×tamp=1486486510)
Picha aliyopost Ommy Dimpoz ikiashiria kuwa huyo ndiye mpenzi wake
Ommy Dimpoz alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz cha EATV wiki kadhaa zilizopita, Ommy alifunguka na kuthibitisha kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano na raia wa China., ambaye watu wengi hawamjui.
Juzi Ommy Dimpoz ametupia Instagram picha ya pamoja akiwa na binti huyo mwenye asili ya China kisha akaweka 'emoji' yenye ishara ya love, akiashiria 'Mapenzi bampa 2 bampa'.
Ingawa Ommy Dimpoz hakutaka kufungua mjadala kwenye picha ile kwa kuamua kufunga uwanja wa comment ili watu wasiweze kuzungumza wala kujadili katika picha hiyo. Lakini ukweli ni kwamba picha ile inazungumza mambo mengi kwa kila anayeiangalia.
Ommy Dimpoz