Wednesday , 10th Dec , 2014

Staa wa muziki anayefanya vizuri kutoka Arusha Tanzania, Hisia baada ya kujiweka vizuri katika soko la muziki akiwa na rekodi rasmi zipatazo tatu, amezungumzia suala la maudhui ya ngoma zake kugusia mapenzi tu.

msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Hisia

Hisia ameweka wazi kuwa, rekodi zinazohusu mambo mengine zipo isipokua kuachiwa kwake kunahitaji mipango na akiwa kama msanii anaona dhahiri kuwa suala zima la mapenzi katika muziki hugusa hisia za watu na pia kuuza haraka tofauti na rekodi ambazo huwa zinazungumza juu ya mambo mengine ya kijamii.