Harmonize ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba producers wasipende kujilimbikizia kazi nyingi peke yao, kwani inashusha ubora wa kazi.
“Nimegundua kitu kimoja, sio lazima kila kitu ufanye mwenyewe, kwa sababu unavyokodisha watu wa light ambao ni profesional, ukikodisha na watu wengine ambao ni profesional vitu vinazidi kwenda kiprofesional zaidi mwisho wa siku tunapata kazi nzuri tunafikisha muziki wetu mbali, tusing'ang'anie kila kitu tufanye sisi wenyewe, kuwapa nafasi watu tofauti katika production yako kunaweza kusaidia muziki wetu kufika mbali”, alisema Harmonize.
Pamoja na hayo Harmonize amewataka wadau mbali mbali na serikali kuwezesha upatikanaji wa maeneo ya kufanyia shooting ya video, ili kuepuka kwenda kufanya kazi nje na kuingia gharama kubwa.
“Kwa upande wa serikali au watu wamiliki wa sehemu mbali mbali za location, tujaribu kuamini kuwa muziki ni kitu ambacho kinaweza kutufuta majonzi kwa sababu ukiangalia mpira haufanyi vizuri, sehemu kibao hazifanyi vizuri, muziki ni kitu peke ambacho tunajivunia, so tujaribu basi kulegeza sehemu za location ziwe rahisi, usidhani kama tunapenda kufanya video nje ila kuna vitu vinapatikana kirahisi”, alisema Haronize.
Akihitimisha hilo Harmonize amesema anapenda kuona watu wa hapa nyumbani wanajiongeza na kufanya vitu vyenye ubora, ili kuweza kupata kazi nzuri na kutangaza zaidi muziki wetu.
“Ningependa kuona upande wa madirector wetu wa kibongo wanafanya video nzuri ambazo zitakuwa zinazidi kuvuka ng'ambo, haina maana kwamba hawafanyi video nzuri, lakini tujaribu kujiongeza zaidi kwa sababu wenzetu tunaona production za nje zinafanya vizuri, ukiangalia top 10 ya tv mbali mbali unaona video za madirector wa nje nyingi sana zinafanya vizuri japokuwa na za kwetu pia zipo, lakini ilitakiwa sisi tuwe na nafasi kubwa”, alisema Harmonize.



