Young Dee ametoa kauli hiyo baada ya watu wengi kuwarushia lawama ma-producer kwa kusema wao ndiyo wanasababisha kufanya muziki wa sasa kutokuwa na ushindani katika 'game' na kusema kuwa wasanii wengi wanaimba nyimbo ambazo hazina mashairi mazuri na kufanya nyimbo hizo kutofika mbali.
"Hamna ushindani kabisa sasa hivi kwenye muziki wa bongo fleva....Sasa hivi zinatoka nyimbo 20, unapita wimbo mmoja unasema kuna ushindani ?...Inatakiwa ukisema kwenye ushindani nyimbo 20 kama tano zinakimbizana ambazo unaweza kusema kuna ushindani...Watu wamerelax sana, muziki una watu wengi ila hakuna ushindani". Alisema Young Dee
Hata hivyo kauli hiyo ya Young Dee inafananishwa na ile aliyoitoa msanii mkongwe,Makamua kwa kusema 'game' ya sasa imekuwa kama ‘buble gum’ kulingana na wanachokifanya wasanii wengi kwenye game.