Wednesday , 26th Feb , 2014

Msanii mkali kabisa wa muziki kutoka nchini Kenya, Habida ameamua kuweka nguvu zaidi katika kuonyesha kipaji chake kingine kikubwa cha kuigiza, ambapo ameshiriki katika Tamthilia ya muendelezo ya New Beginnings bado ipo katika matayarisho ya mwisho.

Mwanadada huyu amewataka mashabiki wake kukaa tayari kwa ujio wake huu mpya ambapo amesema kuwa, amejisikia poa kupata nafasi hii ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza.

Habida kwa upande wa kazi zake za muziki, amerudi tena kwa kasi akiwa akiwa na ngoma mpya inayokwenda kwa jina I Love You iliyofanyiwa 'mixing' upya na Dj Sabby, akiwa amemshirikisha Flabba pamoja na Jovislash.