Friday , 12th Sep , 2014

Rapa mkali kutoka kundi la Weusi, G Nako ambaye hivi karibuni alikwenda kufanya kazi kadhaa za muzikinchini Kenya, amesema kuwa, amejionea utofauti katika ufanyaji kazi huko, suala kubwa likiwa ni utunzaji wa muda wa kazi.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini G Nako

G Nako ameweka wazi kuwa, katika ziara hizi ameweza kufanya kazi kadhaa na wasanii kutoka huko, amesema kuwa, tofauti na hapa nchini, nje ya nchi ratiba ya studio inakuwa inazingatiwa sana.