Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mx Carter amesema Fid Q ni mtu ambaye yuko real sana, hivyo hata wanapofanya photoshoot inamuwia vigumu kupata picha nzuri, hivyo iwapo mwanafunzi ataweza kumpiga picha nzuri Fid Q, basi hakuna mtu atakayeshindwa kumfanyia kazi nzuri.
“Unajua mtu kama yule pale kwenye touch anakuwa anakupa mwanga mzuri wa kumtouch vizuri, mtu anajifunza zaidi, mtu kama Joh unajua yupo kawaida, picha yake ukimpiga haikupi hata kazi, kwa hiyo hata kwenye kujifundisha huwezi kumtumia Joh Makini, Fid Q ukimpiga picha na uko na mwanafunzi inakuwa fresh, hata kumfundisha mtu Fid ndio anafaa, mpaka umfanye picha yake ikubalike inakuwa ngumu sana”, amesema Mx Carter.
Mpiga picha huyo pia ni mtu wa karibu wa wasanii wengi bongo, kutokana na uwezo wake mkubwa kwenye masuala ya mitandao.
