Friday , 21st Mar , 2014

Msanii Slim Fahrenheit kutoka wa Jijini Nairobi nchini Kenya, ameweka wazi ujio wa kazi yake mpya ambayo ni kolabo aliyofanya na Prezzo, kazi ambayo amejitapa kuwa, katika kutengeneza video yake, location 1 kwa saa 1, imegharimu 300000Kshs.

Fahrenheit amesema kuwa, video hii itahusisha ufahari wa hali ya juu ikiwepo matumizi ya Private Jet na vitu vingine vinavyoonyesha maisha ya gharama kwa ajili ya kuifanya video hii kuwa katika kiwango cha Kimataifa.

Baada ya taarifa hii, kwa sasa mitaa inasubiri kwa hamu kuona ni nini mastaa hawa wanaopenda kushine zaidi, watakifanya wakati ambapo video hii ya gharama itakapokamilika na kutoka.