Wednesday , 31st Aug , 2016

Msanii Bebe Cool wa Uganda amezizungumzia 'EATV AWARDS' kuwa ni kitu kizuri na chema kwa wasanii wa Afrika Mashariki

Akizungumza na East Africa Television kwa njia ya simu, Bebe Cool amesema tuzo hizo zimetoa fursa ya kuwaunganisha wasanii wa nchi hizo tatu, ambao kwa sasa wamekuwa kama wametengana kwenye kazi. 

"It is a good thing because it brings more connection which we had before it was disconencted, there was a conection in East African Music Industry before, things like such awards is the one which will conect back the industry, musician get together, film industry get together  as East African, any one who won an award will be representing to one country,  but for the moment i think it will be very interesting to put all together .......akimaanisha (Ni kitu kizuri kwa sababu kinaleta zaidi muunganiko ambao tulikuwa nao kabla haujavunjika, kulikuwa na muunganiko kwa wasanii wa tasnia ya muziki Afrika Mashariki, vitu kama hizo tuzo ndiyo kitakachounganisha tena tasnia,wanamuziki kuwa pamoja, tasnia ya filamu kuwa pamoja, ila kwa sasa nafikiri ni kitu kizuri, na yeyote atakayeshinda atawakilisha nchi moja, itakuwa vizuri kuwaweka wote pamoja", alisema Bebe Cool.

Bebe Cool ambaye ni msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki, amesema tasnia ya muziki Afrika Mashariki ilikuwa na ushirikiano mzuri, lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti na siku za nyuma.

Tags: