Wednesday , 28th Sep , 2016

Msanii Baranaba Elias amewataka wasanii wenzake kutodharau zoezi la uchukuaji fomu na kushiriki EATV AWARDS, na kusema ni kitu cha msingi kwao.

Barnaba

Akizungumza na East Africa Television, Barnaba amesema baadhi ya wasanii wamekuwa wakizichukulia poa tuzo hizo kuwataka kuacha kuzipuuza na badala yake wachangamkie zoezi la uchukuaji wa fomu za kushiriki katika tuzo hizo.

"Mi nishachukua najaza sasa hivi nadhani wiki ijayo nitarudisha, wasanii wenzangu wasidharau, wakachukue fomu za kushiriki tuzo, hii ni fursa kwetu", alisema Barnaba.

Barnaba aliendelea kusema kuwa tuzo hizo ni kitu kizuri kwao kwani kinaleta 'exposure kwenye tasnia ya sanaa, na pia inaleta changamoto kwenye kazi zao.

"Hii ni nafasi nyingine kwetu wasanii kutambua mchango wetu, inaleta changamoto, hafla kama hizi inaleta competition kwenye game na ni nzuri pia", alisema Barnaba.

Barnaba ambaye kwa sasa anaendelea kufanya poa kwa wimbo wake mpya wa 'Lover Boy', ni miongoni mwa wasanii ambao wamethibitisha kushiriki tuzo hizo kwa kuchukua fomu za kushiriki, zinazopatikana kwenye tovuti ya https://www.eatv.tv/awards au katika ofisi za EATV zilizopo Mikocheni Dar es Salaam.

Tags: