
Katika kusherehekea miaka 17 ya utendaji kazi wa kituo cha East Africa Radio, kituo kiliandaa show ambapo wasanii kama Ommy Dimpoz, Mwana FA, Shilole,Belle 9 na Dully Sykes walionyesha ukomavu wa kutawala jukwaa katika kutoa burudani kwa wakazi hao.
Alipo panda Dully jukwaani umati ulizizima alipopiga nyimbo zake za zamani kama 'Lady is free', 'Bongo Flava' na 'Handsome' ambapo watu walionekana kuzikumbuka vyema na kuimba naye mwanzo mwisho.
Aidha tamasha hilo lilidhaminiwa na East Africa Radio ili kuwezesha wananchi kufurahia burudani bure, na ili kujua eneo linalofuata kwa sasa endelea kuisikiliza matangazo na vipindi bora toka East Africa Radio.
