Tuesday , 2nd Aug , 2016

Moja kati ya waimbaji wa bend ya Yamoto Bend Dogo Asley amesema sababu iliyopelekea kutoa ngoma yao mpya ya Mijudo ni kutokana na nadhiri waliyoiweka tangu zamani

YAMOTO BEND

Akipiga stori na eNewz Asley amesema “Tumetoa ngoma yetu mpya kwa sababu ilikuwa ni nadhiri yetu, tulisema ikifika miaka mitano ya Mkubwa na Wanawe ni lazima tutoe wimbo”.

Hata hivyo Dogo Asley alisema watu wasielewe vibaya kama wanavyohisi kwamba ngoma yao iitwayo SUU walioifanya na Ruby haijakubalika na ndio sababu wakaamua kutoa nyimbo nyingine bila kuchelewa.