Thursday , 31st Dec , 2015

Akiwa anaendelea kufurahia ujio wake wa pili hapa nchini, Dj Young Guru kutoka nchini Marekani ameelezea kuhusiana na uzoefu alioupata baada ya kufanya kazi na nyota wa muziki Jay Z pamoja na Alicia Keys kupitia wimbo wa 'Empire State of Mind'.

Dj Young Guru kutoka nchini Marekani ambaye yupo nchini Tanzania

Dj huyo Gimel Androus Keaton aka Young Guru, ambaye pia ni mhandisi wa sauti na pia mtayarishaji wa muziki, ameongea na eNewz kuhusiana na safari yake fupi, kuingia katika sekta hiyo ya uhandisi wa sauti hadi kufikia kilele cha kushirikiana na mastaa wakubwa wa muziki.

Staa huyo anaungana na nyota wa muziki Tekno Miles, kutoka nchini Nigeria ambao leo hii watauwasha moto wa burudani kali katika onesho la muziki lililobatizwa jina 'Grown & Sexy' litakalofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika mkesha wa kuufunga mwaka 2015 na kuufungua mwaka mpya wa 2016.