Monday , 16th Mar , 2015

Baada ya mapokezi mazuri ya kazi yake mpya ya Wanjera, staa wa muziki Ommy Dimpoz ambaye ameendelea kupokea sifa na maoni tofauti kutokana na kazi hiyo amesema kuwa amejifunza kwa asilimia 70, jinsi ya kutengeneza stori katika video.

msanii wa miondoko ya bongofleva Ommy Dimpoz

Staa huyo amesema kuwa, video yake ya Wanjera mpaka sasa yeye binafsi hachoki kuitazama kutokana na kisa chake, sehemu anazokubali zaidi zikiwa ni zile alizofanya Idris.