Ivrah
Akiongea kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' Ivrah amesema kwa sasa anatamani kufanya kazi sana na kuhakikisha anafikia level ya kina Diamond pamoja na Alikiba kimuziki ambapo watu wanakuwa wakiwatolea macho wao pekee na kuwazungumzia ikiwa pamoja na kuwashindanisha kimuziki.
"Diamond na Alikiba wote wawili wananipa mimi kizunguzungu nataka na mimi nifike pale walipo wao ambapo watu wanawashindanisha huyu na huyu nani mkali, ndipo napotaka mimi kufika pale" alisema Ivrah