Wednesday , 29th Apr , 2015

Staa wa muziki wa nchini Uganda, Desire Luzinda baada ya tishio la kufutwa kwa ziara yake kubwa huko Afrika Kusini kutokana na machafuko ya Xenophobia, hatimaye ameelekea nchini humo kuweka mambo sawa.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Desire Luzinda

uwepo wa Desire nchini humo, umekuwa pia ni nafasi ya kuonesha ulimwengu kuwa hali hiyo ya machafuko imedhibitiwa na pia kurejesha imani na upendo kwa taifa hilo ambayo ilianza kupata madoa nje ya mipaka yake.

Desire atatumbuiza nchini humo tarehe 30 mwezi huu kabla ya kuelekea Dubai na baadaye Marekani kuendelea kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki.