Monday , 30th May , 2016

Wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva wakutana kusherekea kumbukumbu ya msanii mwenzao Albert Mangwear ikiwa ni miaka mitatu tangu msanii huyo afariki dunia akiwa nchini Afrika Kusini.

Kumbukumbu hiyo ambayo iliandaliwa na wasanii kutoka katika kundi la Rada Entatainment linalomilikiwa na T.I.D Mnyama lilikutanisha wasanii mbalimbali kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo kwa pamoja wakishirikiana na mashabiki zao ambao walipata shoo kutoka kwa wasanii tofauti tofauti waliohudhuria kumbukumbu hiyo.

Wasanii waliokuwa wamejitokeza katika kumbukumbu hiyo ni pamoja na Mirror, Nyandu Tozi, Country Boy, Jordan, Jay Mo, Linex, Dudu Baya na wengineo ambao wote kwa pamoja walionekana kufurahia tukio la kumbukumbu ya kifo cha msanii mwenzao.