Saturday , 26th Apr , 2014

Mwanamuziki wa kimataifa kutoka nchini Jamaica, Demarco ambaye anatarajia kufanya onesho la aina yake nchini Uganda, ameonesha kupania kufanya kitu cha aina yake siku ya onesho, baada ya kutanguliza timu yake nchini humo kwa maandalizi.

Demarco

Demarco akiwa anafanya kazi kwa karibu na meneja wake, Karl Palmer pia ameamua kuituma timu hii kabla yake kwa kazi ya kukagua vifaa na eneo la tukio, sambamba na kuhakikisha kila kitu ambacho yeye na waratibu wa onesho wamekubaliana katika mkataba kinatimizwa.

Msanii huyu mwenyewe, anatarajiwa kutua nchini Uganda tarehe 8 Mwezi Mei, kwaajili ya onesho lake kubwa kabisa tarehe 10 katika ziara hii ambayo anatarajia kuitumia pia kutengeneza kazi kadhaa na wasanii wa Uganda.