
Dayna Nyange
Akipiga story ndani ya eNewz ya EATV amesema "siyo vibaya kuandikiwa wimbo lakini kwa wakati mwingine ni vizuri kujua kujiandikia mwenyewe kwani unaweza kupata zali la kuingia studio kubwa hata nje ya nchi na kupata nafasi ya kurekodi hata na wasanii wakubwa ukashindwa na ukapoteza zali kwa kuwa hujui kuandika".
Pia Dayna hakusita kumwagia sifa msanii mwenzake Maua Sama kwani anadai aliwahi kusikia kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike wanaoweza kujiandikia nyimbo na kumsifia kwamba ni mwandishi mzuri.