Monday , 17th Nov , 2014

Msanii anayefanya muziki wa miondoko ya Soul hapa nchini, Damian Soul amesema kuwa aina ya muziki huo ndio njia pekee ambayo anaona yeye anaweza kuutumia kufikisha ujumbe wake, na anafurahi kuona mapokezi yake yakiongezeka siku hadi siku.

msanii wa muziki wa miondoko ya Soul nchini Tanzania Damian Soul

Damian amesema kuwa amepata nguvu ya kuendelea kufanya zaidi muziki huu baada ya kuona mashabiki wakikubali katika majukwaa makubwa, ingawa bado mtindo anaofanya unachanganywa na muziki wa Bongofleva.

Ni Penzi featuring Joh Makini, ndio mzigo mpya kutoka kwa Damian, na hapa anaelezea staili yake hii ya Muziki.