Saturday , 25th Apr , 2015

Rapa D Knob ambaye ana nafasi yake kubwa katika historia ya game ya Hip Hop Bongo, ameeleza juu ya kuwa na wazo la kuanza kusimamia wasanii chipukizi wenye vipaji, ili kuwaweka katika ramani ya game.

D Knob

D.Knob akiwa kwa sasa amejikita zaidi katika shughuli zake binafsi pembeni ya muziki amesema kuwa, amekuwa na wazo hilo kwa muda akiona umuhimu wa kufanya hivyo kuendelea kutoa mchango wake katika muziki hapa Bongo, mpango ambao unahitaji uwekezaji mkubwa, na hapa anaeleza zaidi mwenyewe.