
Country Boy
Country Boy alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusema wimbo huo ni moja ya ngoma anayoikubali zaidi tangu ameanza kufanya kazi na kushirikiana na wasanii wengine na kusema anaupenda wimbo huo kwa kuwa una ujumbe ndani kuwa hata watu wakibana vipi mdogo mdogo watasonga na kufikia malengo.
Mbali na hilo Country boy amedai kwa sasa anajipanga kuachia video ya wimbo huo ambayo huenda ikatoka mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi wa pili.