Thursday , 6th Aug , 2015

Colonel Moustapha, staa wa muziki mwenye matukio ya kushika hisia za watu mara kwa mara kutoka Kenya, safari hii ameweka dhahiri kutekwa katika penzi jipya na mwanamke ambaye bado hajawa tayari kumuweka wazi.

Staa wa muziki nchini Kenya Colonel Moustapha

Kwa njia ya mtandao msanii huyo ameanza kuziweka picha za mpenzi wake huyo sambamba na jumbe mbalimbali za kuonyesha namna alivyozama katika penzi hilo, bila kuonyesha sura ya mwanamke huyo.

Staa huyo alivuma sana kipindi cha nyuma akiwa katika penzi na msanii mwenzake, Marya ambaye hata hivyo hawakuweza kudumu zaidi, na amekuwa akiyumba yumba kimapenzi mpaka sasa ambapo amekuwa na ujasiri wa kuanza kulitambulisha penzi lake jipya kwa mashabiki wake.