Tuesday , 8th Apr , 2014

Kupishana kwa maelewano kati ya msanii Nyota Ndogo dhidi ya Colonel Moustapha, kumeendelea kutikisa vichwa vya habari baada ya Nyota Ndogo kukerwa na kauli ya hasimu wake huyu kuwa kuna kitu zaidi ambacho yeye anakitaka kwa Colonel.

Colonel Moustapha

Hii ni kufuatia kauli ambayo Colonel aliitoa wakati akimuomba Nyota Ndogo msamaha kwa kosa la kutumia picha zinazodhalilisha wanawake kujitangaza kimuziki, ambapo alisema kuwa vita ambayo Nyota Ndogo amemuanzishia ina sababu nyingine zaidi ya madai ya kukerwa na picha mbovu alizopiga.

Kutokana na kauli hii ya Colonel, Nyota Ndogo amesema kuwa yeye ameamua kukaa kimya baada ya kuombwa msamaha, lakini anashangaa kuwa hasimu wake huyu anaendelea kumtafuta maneno.