Wednesday , 14th Dec , 2016

Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola imewataka wasanii na vijana wenye vipaji kuitumia programu yao ya Coke Studio ili kujijengea uwezo wa kushinda tuzo kubwa duniani ikiwemo zikiwemo tuzo za EATV.

Usiku wa Tuzo za EATV

Maneja Masoko kutoka kampuni hiyo Bwana Peter Mpalla ambaye alikuwepo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo katika ukumbi wa Mlimani City dar es Salaam, amesema lengo la Cocacola ni kuendeleza vipaji nchini Tanzania kupitia muziki, mpira wa miguu na ndiyo maana ikiaamua kushiriki katika tuzo hizo.

Pia amesema kuwa Tuzo hizo ni moja ya matunda ya watu waliopitia Coke Studio, programu ambayo inawafundisha na kuwajenga wasanii ili kuwa na uwezo waAkuchukua tuzo kubwa kama hizi.

Amewataka vijana wenye vipaji kuitumia vizuri Coke Studio ili kufikia malengo yao katika sanaa.

Msikilize hapa;- 

 

 

Tags: