Saturday , 28th Jun , 2014

Staa wa muziki wa nchini Uganda, Mwanadada Cindy Sanyu amenyanganywa haki ya malezi ya binti yake baada ya baba wa mtoto huyo, Mario kufanikiwa kuishawishi mahakama kuwa yeye ndiye mtu sahihi wa kuweza kumlea mtoto huyo baada ya wawili hawa kutengana

Mario na Baba Mtoto wake, Mario

Katika utetezi wake mahakamani, Mario ameeleza kuwa, Cindy amekuwa na ratiba kali inayohusisha showz kadhaa za muziki nje ya nchi, na hivyo kumfanya mwanamama huyu kuwa na muda mchache wa kukaa na mwanae.

Bado haijafahamika kama Cindy ataendelea kupambana kisheria na Mario kuhusiana na swala hili baada ya kueleza kuwa mwanae huyu anaweza na amezoea kupewa malezi mazuri na mama yake pindi yeye anapokuwa katika shughuli zake za muziki.

Tags: