Sunday , 29th Nov , 2015

Nyota wa miondoko ya gospel nchini Christina Shusho, anatarajia kuwapa mashabiki zawadi ya X-mas kwa kuachia wimbo mpya wiki hii.

Nyota wa miondoko ya gospel nchini Christina Shusho,

Nyota huyo anayezidi kung'aa kupitia nyimbo yake mpya inayofanya vyema iliyobatizwa jina 'Im gonna work for the Lord' ameongea na enewz kuwa hii itakuwa ni zawadi kubwa kwa mashabiki wake kwa ajili ya kuelekea katika sherehe hiyo kubwa ambapo ameelezea nia na madhumuni ya kuachia wimbo huo mpya uliobatizwa jina 'Waranda randa Mbao'.