Wednesday , 17th Jun , 2015

Staa wa muziki Chegge Chigunda ameweka wazi kuwa baada ya kuona ukubwa na mafanikio ya projekti y

Chegge

Staa wa muziki Chegge Chigunda ameweka wazi kuwa baada ya kuona ukubwa na mafanikio ya projekti ya filamu aliyofanya huko Nairobi, katika siku zijazo ataanza kuonekana katika Tamthilia ya Muendelezo ama Series ya kazi hiyo ambayo ilifanyika miaka kadhaa iliyopita.

Chegge ambaye hivi sasa anatamba katika chati mbali mbali kupitia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina 'Mwananyamala', ambaye ameeleza kuwa atatanguliza projekti ya awali ya kazi hiyo ambayo imekwishakamilika, anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa upande huo wa uigizaji.

Kuhusiana na kazi hii, kwa kifupi hapa Chegge anafafanua.