Thursday , 19th Jun , 2014

Wasanii wanaoliunda kundi maarufu la muziki wa bongo flava nchini TMK Wanaume Family Chege na Mh. Temba wanatarajia kuachia kichupa chao kipya walichokibatiza jina 'WAUE" ambacho kinatarajiwa kutambulishwa kesho Ijumaa jijni Dar es Salaam.

Wasanii wa kundi la TMK Wanaume Family

Kichupa hicho kipya kimefanyiwa kazi safi na Adam Juma pia kwa upande wa audio kimetengenezwa katika studio za Wakubwa na Wanawe chini prodyuza Marco Chali.

Said Fella amesema kuwa hii itakuwa ni zawadi kwa mashabiki na wadau wa muziki kwani Chege na Temba wamekuwa ni wasanii ambao wako imara na hufanya kazi bila kubahatisha.