Charz Baba akiwa na mkewe na watu wake wa karibu
Imefahamikwa kwamba mwanadada huyo huenda angeolewa na Alikiba endapo asingekwenda kuoa Mombasa.
Charz amesema hajui chochote kuhusu mahusiano ya Alikiba na mke wake na anachokijua yeye ni kwamba mke wake na familia ya Kiba zina ukaribu na ndio maana hata katika harusi ya mdogo wake Ali, Zabibu Kiba, mwanadada huyo alikuwa mtu wa karibu sana katika kukamilisha harusi hiyo.
"Nimeamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite na ukitaka kumchunguza bata utashindwa kumla utaishia kutapika,mapenzi yanamambo mengi sana ukitaka kuyafatilia yote huwezi kukaa kwenye ndoa mimi na mke wangu kila mtu anamadhambi yake ila tulikaa chini tukaamua kuachana na ya nyuma na kuanzia familia yetu", amesema Charz Baba.

Pia Charz alimalizia kwa kusema kitendo cha Ali Kiba kuja na kuimba kwenye harusi yake hiyo inadhihirisha wazi kwamba roho yake ni nyeupe na hana tatizo lolote na mke wake hivyo kwa sasa wanaishi na mke wake kwa upendo na amani na hakuna kati yao anayeangalia historia ya zamani ya kimapenzi kati yao.
Tazama zaidi hapa chini Charz Baba akizungumza.





