
Chameleone amepewa jukumu hili na Spika wa Bunge la nchini Uganda, Mheshimiwa Rebecca Kadagaa mbaye amesema kwa nafasi ya msanii Jose Chameleone kwa sasa katika ngazi ya kitaifa na
kimataifa, ana uhakika kuwa msanii huyu atafanya kazi yenye manufaa makubwa.
Msanii huyu pia amekabidhiwa ubalozi wa shindano maalum la kutangaza utalii la Kupanda Mwamba wa Kagulu katika Mkoa wa Buyende kwa mwaka huu, ambapo watu mbalimbali watashiriki shindano hili siku ya tarehe 9 na 10 mwezi Mei.