Friday , 9th May , 2014

Msanii Jose Chameleone ambaye ni balozi wa mahusiano mema wa Utalii huko Busoga Uganda, anatarajia kushiriki katika zoezi la kupanda Mlima Kagulu huko Buyende Uganda, kama moja ya jitihada za kuhamasisha utalii wa ndani wa nchi hiyo.

Chameleone na spika wa bunge la nchini Uganda, Rebecca Kadaga

Katika zoezi hili Chameleone atashirikiana na Rais Museveni na vile vile spika wa bunge la nchini Uganda, Rebecca Kadaga, ambao wote hawa wataoneshana umahiri katika tukio hili ambalo pia ni mazoezi tosha kwa mwili.

Msanii huyu ambaye ndio kwanza ameachia video mpya ya ngoma yake inayokwenda kwa jina Gimme Gimme, kwa kipindi cha mwaka mzima atakuwa akifanya shughuli hii ya Ubalozi wa mahusiano mema katika sekta hii ya utalii.

Tags: