Friday , 8th Aug , 2014

Msanii wa muziki Jose Chameleone kutoka nchini Uganda, amesema kuwa, amekuwa akijituma sana katika kazi mbali mbali, umiliki wa nyumba na viwanja, na biashara ikiwepo ya madini na kilimo.

msanii Jose Chameleone wa Uganda

Chameleone amekiri kuwa jitihada zake hizo ndizo ambazo zimeweza kumuingiza katika orodha ya wasanii 10 matajiri zaidi barani Afrika.

Katika mahojiano maalum aliyofanya na eNewz, amesema kuwa, licha ya kuwa na vyanzo vyote hivi vya mapato, yeye anapenda mashabiki wake kumchukulia yeye kutokana na muziki na si biashara.