Wednesday , 17th Dec , 2014

Msanii wa muziki Jose Chameleone, amefanya mkutano na waandishi wa habari kuelekea onyesho lake kubwa la One Man show ambalo kabla ya mabadiliko kingilio chake kilikuwa ni shilingi za Uganda milioni 1.

msanii wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone

na kusema kuwa

Chameleone amejitetea kuwa kushusha bei ya tiketi hizo ni kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi kuhudhuria, hivyo ameamua kuweka madaraja ya tiketi ambapo zitapatikana pia kwa shilingi za Uganda laki 2 na laki 5, na hii si kwa ajili ya kuhofia kubuma kwa onyesho, bali ni kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya shughuli za hisani kufikishia wananchi maji huko Karamoja.

Chameleone amesema kuwa, kwa atakayehudhuria onyesho hili moja kwa moja anakuwa ameshiriki katika shughuli hii ya hisani na vilevile kujipatia nafasi ya kupata burudani ya aina yake kwa kufungia mwaka.