Monday , 1st Feb , 2016

Meneja wa kundi la Yamoto Band kutoka Mkubwa na Wanawe, Chambuso ametolea ufafanuzi kitendo cha kutambulisha kundi jipya la Salam katika game ya Bongo Fleva, wakati ikionekana dhahiri kuwa muziki wanaofanya ni ule ule ambao unafanywa na Yamoto Band.

Said Fella na Meneja Chambuso

Chambuso amekiri kuwa, wao kama wasimamizi, akiwepo pia Temba, Fella na Salam wameiona changamoto hiyo kubwa, na wanajaribu kuifanyia kazi ili kuleta ladha na bidhaa tofauti kwa wapenzi wa burudani.

Chambuso pia ameeleza kuwa, lengo la kutambullisha kundi hilo jipya ni kutoa fursa zaidi kwa kundi kubwa la vijana waimbaji kutoka Mkubwa na Wanawe ambao wanazidi 40, na hawana mpango wa kuiua wala kuiletea ushindani Yamoto Band.

Chambuso pia amesema kuwa, kundi hilo la Salam linafanya muziki wake kwa kupita njia zile zile za Yamoto Band kutokana na kuwa wanafundishwa muziki na vijana machachari wa Yamoto Band.