C9
Mtayarishaji muziki C9 kutoka studio yake mwenyewe ya C9 Records, ameeleza kuwa mwaka huu ameamua kurejea kwa kasi katika kutayarisha ngoma za Hip Hop, baada ya kufanya Bongo Fleva na kusitisha kwa muda na baadaye kujikita katika muziki wa dansi, taarab na mahadhi mengine, kitu ambacho kimesababisha jina lake kufifia kwa upande wa muziki wa kizazi kipya.
C9 ameeleza kuwa, kwa sasa tayari amekwishaanza kufanya kazi studio na wasanii wakubwa akiwepo Young Dee kuweka alama ya kurejea kwake, akiwa hapa ananyoosha mwenyewe maelezo kuhusiana na suala hilo.
Mtayarishaji muziki huyo pia, akagusia suala la kipato ambacho kimekuwa ni kidogo kwa upande wa muziki wa kizazi kipya, hii ikiwa ni moja ya sababu ya yeye kuuweka benchi kwa muda.





