Sunday , 29th Jun , 2014

Msanii Burna Boy wa nchini Nigeria anatarajia kutumbuiza katika tamasha maarufu la muziki wa Reggae liitwalo The Annual Reggae Sumfest litakalofanyika mwezi July mwaka huu huko Montego Bay, nchini Jamaica.

Msanii wa muziki nchini Nigeria, Burna Boy

Burna Boya ambaye pia anakamilisha michakato ya kurekodi wimbo na msanii maarufu wa nchini Tanzania Vanessa Mdee,anatarajia pia kufanya kolabo na msanii Beenie Man wa nchini Jamaica

Aidha mkali huyo ameachia single yake mpya aliyoibatiza jina 'Don Gordon' jijini Nairobi, ukiwa ni wimbo wa ujio wa albamu yake mpya baada ya kutoa ya awali iitwayo L.I.F.E.