Friday , 8th Aug , 2014

Mwigizaji Brenda Wairimu kutoka nchini Kenya ameendelea na kampeni yake aliyoipatia jina Beat Cancer kwa ajili ya kuongeza uelewa wa watu kuhusiana na ugonjwa huu mkubwa.

muigizaji wa nchini Kenya Brenda Wairimu

Katika jitihada zake mpya, Brenda amesema kuwa kwa sasa ameamua kuelekeza jitihada zake hizi katika kusaidia watoto wanaougua ugonjwa huu huko Kenya, ambapo amewataka makampuni mbalimbali kujitokeza pia kusaidia.

Brenda ameweka wazi kuwa, kujiingiza kwake katika harakati hizi ni kutokana na kuguswa na namna ambavyo ugonjwa huu umeathiri wanafamilia wa rafiki zake wa karibu kabisa.