
BowBow
Kiyomi Leslie amefungua mashtaka hayo kwa rapa huyo baada ya kupost malalamiko katika mtandao wa Twitter, juu kunyanyaswa kimwili kwa kupigwa na Bow wow huku akiwa na kiumbe tumboni.
"Alinipiga wakati nina ujauzito, alinipiga ngumi za tumboni na mwili mzima , nilimpoteza mwanangu nilikua dhaifu sana kwake."
Hata hivyo mwanamke huyo amelalamikia kuwa, alikuwa anapigwa mara kwa mara na rapa huyo, ashampokonya simu yake na kuitupa na pia aliwahi kumfungia mlango chumbani na kutomruhusu atoke.
Wawili hao walianza mahusiano mwaka 2017 na kuachana Februari 2019 baada ya kupigana. Bow wow ameshakuwa na mahusiano na Ciara, Keyshia Cole, Erica Mena na Keyomi Leslie na wote aliachana nao kutokana
vurugu zake.