Tuesday , 8th Sep , 2015

Moja kati ya wasomi wakubwa wanaofanya muziki wa Hip Hop hapa Bongo, Dr. Godfrey Nyahongo maarufu zaidi kama Bonta Maarifa kutoka kundi la Weusi ametoa tathmini yake juu ya mulekeo, misimamo ya wasanii kisiasa.

mkali wa miondoko ya Hip hop nchini Tanzania Bonta Maarifa

Bonta amewataka mashabiki kuelewa kuwa wasanii wana haki zote za kusimama upande wowote kisiasa wakiwa kama raia wengine wa kawaida.

Mkali huyo pia ametaka wasanii hao kufahamu tofauti zao kama raia wa kawaida, na katika nafasi zao kama wasanii ambao wana kundi kubwa la watu nyuma yao wenye mitizamo tofauti, kitu ambacho kwa namna moja ama nyingine kinazua athari kwa kundi lile la watu ama mashabiki.