Thursday , 7th Jan , 2016

Nyota wa filamu Wastara Juma, akiwa moja ya mastaa wanaoguswa na zoezi la bomoa bomoa linaloendeshwa na serikali ambapo nyumba zake mbili zipo katika eneo lisiloruhusiwa, ametoa lawama nzito kwa niaba ya waathirika wote katika zoezi hilo.

Nyota wa filamu Wastara Juma

Wastara amesema, anatoa lawama kwa Serikali akiwa moja ya wananchi walioipigia kampeni kwa nguvu, zoezi hilo likimuacha na mzigo wa watu 28 wanaomtegemea bila makazi akiwa anahitaji matibabu ya pesa nyingi pia.