Saturday , 5th Dec , 2015

Msani Bobi Wine ameamua kujiongeza kwa kuchukua hatua ya kufunga moja ya barabara nchi Uganda, na kuifanyia marekebisho akishirikiana na wasamaria wengine, zoezi zima likihusisha kuondosha shimo kubwa ambalo limekuwa chanzo cha ajali kadhaa eneo hilo

Bobi Wine

Bobi Wine ambaye hatua yake hiyo ilivuta mamlaka inayoendesha jiji la Kampala KCCA ambao walilazimika kuleta greda ambayo ilisaidia kumaliza kazi hiyo, akiwakosoa kwa kuwa mstari wa mbele kusimamia sheria za kufukuza wafanyabiashara wadogo na kukusanya mapato huku wakifumbia macho masuala ya msingi kama hilo.

Nyota huyo ambaye anatambulika kama Rais wa Ghetto, kwa hatua hiyo ametumia maneno kuwa ni jukumu la kila mmoja kuchukua hatua katika kusaidia ama kupambana na masuala muhimu kwa maslahi ya jamii nzima.