msanii wa Uganda Bobi Wine
Bobi Wine ambaye alikuwa na ratiba ya kufanya show kubwa huko Birmingham tarehe 24 mwezi Agosti, sasa huenda asiweze kuingia nchini huko tena, kutokana na kuendelea kushikilia msimamo wake kupinga masuala ya ushoga.
Msanii huyu pamoja na nchi ya Uganda, imekuwa wazi na mstari wa mbele kupinga vitendo vya ushoga, hatua ambayo imekuwa ikiwapatia changamoto na vikwazo kutoka kwa watu, makundi pamoja na nchi zinazounga mkono ushoga.