Wednesday , 27th Jul , 2016

Baada ya muandaaji mkubwa wa muziki wa bongo Fleva kufunga ndoa miezi michache iliyopita mdogo wake wa tumbo moja amekutana na Camera ya eNEWZ na kupiga stori na unaambiwa Manecky siku hizi kawa bosi toka afunge ndoa hashindi tena studio.

Bob Manecky

Bob Manecky ameiambia eNEWZ kuwa “Kwa sasa mimi ndio nashinda studio mda wote kwa kuwa Manecky kwa sasa ni bosi na sisi ndo wafanya kazi wake hivyo yeye huwa anatokea mara chache saana studio."

Pia Bob amesema ni muda sana yeye alikuwa akifanya kazi na kutengeneza bit mbalimbali katika studio ya Manecky japo watu wengi hawakuweza kulitambua hilo na kusema wapo katika marekebisho ya studio yao hivyo wadau watarajie midundo mikali kutoka kwao.