
Mr. Blue
Mr Blue amesema kuwa, kwa muda mrefu sana amekuwa akifanya video za kuunga unga na washkaji, bila kuhusisha gharama zozote kutoka mfukoni kwake, akieleza kuwa Baki na Mimi ndiyo video iliyomsumbua kukamilisha visa vyote alivyoviimba, sehemu ya gharama ikiwa ni kukodisha limousine yenye gharama ya shilingi milioni 1 kwa siku, gauni la zaidi ya shilingi laki 4 na vitu vingine vingi ambavyo amevilipia mpaka kazi nzima ili kuwasilisha kazi nzuri kwa mashabiki.
Blue amesema kuwa, kazi hii inavunja utaratibu wake wa awali wa kuendesha sanaa yake kwa ubahili kidogo, akiwa amejipanga sasa kwaajili ya kuwekeza pesa ili kupata pesa kutoka katika muziki.
